Mfumo Shirikishi wa Kusimamia Utendaji Kazi na Rasilimali za Taasisi
Mfumo huu unatumika kusimamia shughuli za ndani ya taasisi kuboresha utendaji kazi, kusimamia matumizi mazuri ya rasilimali na kuweza kubadilishana taarifa miongoni mwa Idara/Vitengo ili kuoengeza ufanisi, kupunguza gharama za uendeshaji na kutoa huduma bora kutumia moduli 18 zinazowasiliana na kuunganisha shughuli za Idara na Vitengo.
Moduli hizo ni pamoja na Mipango, Bajeti, Uhasibu, Usimamizi wa Wateja, Usimamizi wa Huduma, Utoaji Ankara, Usimamizi wa Rasimaliwatu, Usimamizi wa Likizo, Usimamizi wa Miradi, Usimamizi wa Majukumu ya Watumishi, Usimamizi wa Ununuzi, Mali na Orodha, Usimamizi wa Vitendeakazi, Usimamizi wa Vyombo vya Usafiri, Usimamizi wa watumiaji wa mfumo, Usimamizi wa Taasisi, Usimamizi wa Mfumo wenyewe, na Ripoti
Moduli hii inatumiwa kuwasilisha mpango kazi wa shughuli kwa ajili ya utekelezaji wa mwaka husika na ukamilishaji wa madhumuni na malengo ya kimkakati ya taasisi.
Moduli ya Bajeti inashughulikia matumizi ya fedha kwa mujibu wa shughuli zilizopangwa kwa mwaka husika.
Hii ni moduli inayotunza kumbukumbu za fedha zilizopokewa na kutumika kwa mujibu wa matakwa ya sheria ya fedha za umma na miongozo ya uendeshaji taasisi
Kazi kuu ya moduli hii ni kutunza na kuweka kumbukumbu za mteja kwa kuongeza au kuhariri taarifa za mteja.
Moduli hii inasimamia huduma zinazotolewa na taasisi kwa wateja wake inayoonesha orodha ya huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi.
Moduli hii inatumiwa kuchanganua na kukokotoa gharama ya huduma zilizoombwa na wateja.
Mfumo huu ni nyumbufu, unaweza kubadilika kulingana na mahitaji halisi ya taasisi husika. Pia unaweza kuunganishwa na kubadilishana taarifa na mifumo mikuu ya Serikali kama vile mfumo Mkuu wa Fedha, Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Watumishi (HCMIS), Mfumo wa Malipo ya Serikali Kielektroni (GePG), Mfumo wa Baruapepe Serikalini (GMS) na Mfumo wa Ofisi Mtandao (GeOS).
Mfumo huu unauwezo wa kusaidia shughuli mbalimbali za taasisi na Mfumo huu unasaidia miundombinu mbalimbali ya mifumo. Pia unasaidia baadhi ya mifumo ya ziada ya watumiaji wengine.
Mfumo huu unaruhusu kuongeza au kupunguza moduli kwenye mfumo mkuu bila kuathiri utendaji wa moduli nyingine. Mfumo huu pia unaweza kuunganishwa na kubadilishana taarifa na mifumo mingine yenye viwango vinavyokubalika kimataifa.
Ndiyo, ERMS imetengenezwa katika mfumo ambao unawezesha utekelezaji wa shughuli kuu za kampuni kubwa na zilizogatuliwa katika matawi.
ERMS ina sehemu katika moduli ya uhasibu inayowezesha kurekebisha makosa wakati wa mchakato
Ndio ERMS ni ERP. ERMS imetengenezwa kulingana na mahitaji halisi ya taasisi za kitanzania wakati ERP ni mifumo ambao umetengenezwa kwa kuzingatia mahitaji ya taasisi nyingine nje ya Tanzania hivyo ili utumike unahitaji kufanyiwa marekebisho ili uendane na mahitaji halisi ya taasisi husika.
Ndio , kuna tofati kati ya ERMS na GePG. ERMS inalenga kuboresha utendaji kazi wa ndani ya taasisi ili kuboresha matumizi ya raslimali kwa ufanisi, wakati GePG inalenga kuboresha ukusanyaji wamapato kielektroni kutoka kwa Wananchi kwenda Serikalini.
Tunatoa mafunzo ya awali kwa masaa manne kuhusu mfumo katika ofisi za eGA